Mabantu – Leo Lyrics

Leoooo Mungu ameniona ameniona
Leoooo Mungu ameniona ameniona

Jaza table gonga glass leo mambo yote mneso (amina)
Mungu amekata minyororo ya mateso (amina)
Mvua jua vilitupiga na hatukua na leso (amina)
Ila tuliishi kwa imani tukiamini kesho (amina)
Ukiona yanazidi sana majaribu basi ku succeed kukaribu
Nilianguka nikainuka tena nikajaribu
Nikasema ipo siku mungu atanijibu

Leoooo Mungu ameniona ameniona
Leoooo Mungu ameniona ameniona

Shiiii!!! Nilikua single ila leo niko na bebe (amina)
Nilishalizwaga sana mpaka chozi nikajaza debe (amina)
Tena nabembelezwa nadekezwa dede (amina)
Hatimae leo tumewakata ngebe (amina)
Wakiletaleta mapepo (fire)
Wakitaka tuachane (fire)
Vinenoneno vya chuki
Tukiachana mutuite mbwa tumekaa pale

Leoooo Mungu ameniona ameniona
Leoooo Mungu ameniona ameniona

Yow!! Leo natumia coz jana niliseto (amina)
Ile kupanda kushuka leo nami ninageto (amina)
Dharhau masimango tulishinda mateso (amina)
Tuishi kwa imani na tuamini kesho (amina)
God when say yes nobody can say no
Can say no
Mungu akisema inawezekana nani wakupinga wakupinga? Wakupinga

Leoooo Mungu ameniona ameniona
Leoooo Mungu ameniona ameniona

Comments (0)